Wakati Zlatan Ibrahimovic anarejea katika mji aliokulia wa Malmo, safari hii akiwa mpinzani, wadau wameamua kuonyesha heshima kwake kwa kumkaribisha kwa mfumo wa aina yake.
Jengo refu kuliko yote
katika mji wa Malmo m nchini Sweden limepambwa kwa herufi kubwa ya Z ikiwa na
maana Zlatan.
Zlatan ameshatua Malmo
akiwa na PSG ya Ufaransa ambayo inacheza na timu hiyo Ligi ya Mabingwa Ulaya
leo usiku.
Zlatan amewaambia mashabiki wa Malmo wanaweza kuimba jina lake
kama walivyokuwa wakifanya awali wakati akiitumikia timu hiyo.
Malmo ndiyo ilikuwa timu
yake ya kwanza kubwa iliyomkuza kisoka kabla ya kununuliwa na Ajax ya Uholanzi.
Hajawahi kurejea na
kucheza Malmo akiwa na timu kubwa kama PSG, hii ni mara yake ya kwanza.
Zlatan mwenye asili ya
Yugoslavia alizaliwa katika kitongoji cha Rosenbarg mjini Malmo.
0 COMMENTS:
Post a Comment