Kikosi cha Yanga
kimeendelea na mazoezi ya kujifua chini ya Kocha Hans van der Pluijm.
Mazoezi hayo yamefanyika kwenye
Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam, leo na kocha huyo Mholanzi
aliamua kuachia wachezaji wakipige hasa kama mechi.
Wachezaji walionekana
kucheza wakiwa ‘siriaz’, yaani hakuna utani na ikiwezekana hata ‘kumtandika’
mtu.
Kila upande ulitaka
kushinda na ushindani ulikuwa juu ingawa mara kadhaa Pluijm alisisitiza suala
la kuepuka kumuumizana badala yake kucheza soka la kiume hasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment