Uongozi wa Azam FC, umethibitisha kuwa upo katika hatua za mwisho
za kumsainisha aliyekuwa kipa wa Simba, Ivo Mapunda ambaye kwa muda sasa
amekuwa akifanya mazoezi na kikosi hicho.
Mapunda aliachana na Simba mwanzoni mwa msimu huu, baada ya
uongozi wa timu hiyo kukatisha mpango wa kumsajili licha ya kumkabidhi pesa
zake za usajili.
Katibu Mkuu wa Azam FC, Idrissa Nassor, amesema wanatarajia
kumsajili Mapunda katika usajili huu wa dirisha dogo, hivyo atakuwa ni mchezaji
pekee atakayesajiliwa na timu hiyo kipindi hiki.
“Tupo katika hatua za mwisho za kumsajili Ivo, kwa sasa tupo
kwenye mazungumzo ya kujua tutampa mkataba wa muda gani na mara baada ya
kukubaliana, tutaweka hadharani kila kitu.
“Kwa upande mwingine, wachezaji wetu wote wapo vizuri na hakuna
tutakayemuondoa kwa sasa,” alisema Idrissa.
0 COMMENTS:
Post a Comment