Kikosi cha Taifa Stars
kinaendelea na kambi yake hapa jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa Kocha Mkuu,
Charles Boniface Mkwasa, Stars itafanya mazoezi leo mara moja.
“Mazoezi yatafanyikaa asubuhi
tu, taratibu tumeanza kuwapunguzia wachezaji mzigo.
“Tulianza kwa kasi na
mazoezi yalikuwa magumu sana kwa kuwa tulitaka wawe vizuri,” alisema Mkwasa.
Stars inajiandaa na mechi
dhidi ya Algeria kuwania kucheza Kombe la Dunia hatua ya makundi itakayopigwa
Novemva 14 jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment