Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal
Malinzi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa michuano ya Kombe la
Shirikisho (AzamHD Federation Cup) utakaofanyika leo Jumatatu, saa 9 kamili
mchana katika uwanja wa Karume ambapo timu ya Abajalo FC itacheza dhidi ya
Transit Camp zote za jijini Dar es salaam.
Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi jana kwa mchezo mmoja
kuchezwa katika uwanja wa Karume uliopo mjini Musoma, ambapo Vill Squad ya
jijini Dar es salaam iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3- 1 dhidi ya timu ya
JKT Rwamkoma ya mkoani Kagera.
Katika
uwanja wa CCM Kirumba, Pamba FC ya jijini humo watakua wenyeji wa timu ya
wachimba dhahabu kutoka mkoani Shinyanga, Bulyanhulu FC mchezo utakaoza saa
10:30 jioni.
Jumla
ya timu 64 zinashiriki michuano hiyo kutoka Ligi Kuu, Ligi Daraja la
Kwanza na Ligi Daraja la Pili kuwania kutwaa ubingwa, ambapo Bingwa wa michuano
AzamHD Federation Cup atapata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye Kombe la
Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.
0 COMMENTS:
Post a Comment