Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewatumia
salamu za pongezi wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea
klabu ya TP Mazembe ya Congo DR kufuatia kutwaa Ubingwa wa Ligi ya Mabingwa
Afrika (CL) jana kwa kuifunga timu ya USM Algiers kwa jumla ya mabao 4-1.
Katika salamu zake kwenda kwa wachezaji hao, Malinzi amewapa hongera kwa
mafanikio waliyofikia ya kutwaa ubingwa huo wa vilabu Afrika, na kuwataka
waongeze bidii ili waweze kufanya vizuri pia katika michuano ya Kombe la Dunia
la Mabara litakalofanyika mwezi Disemba nchini Japan.
Malinzi amesema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu na Watanzania
wote wanawashukuru kwa kuiwakilisha vizuri Tanzania kimataifa, na sasa moyo
huyo wa kujituma kwao waundeleleze katika mchezo dhidi ya Algeria wikiendi hii
kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
0 COMMENTS:
Post a Comment