Kiungo mtaratibu aliyewahi kuiliza Yanga mara katika mechi ya Mtani Jembe? Awadhi Juma sasa mkataba wake wa kuichezea Simba
unamalizika.
Awadhi alijiunga na timu hiyo msimu wa
2012/13 akitokea Mtibwa Sugar ambaye mkataba wake wa kuendelea kuichezea timu
hiyo unamalizika mapema Desemba, mwaka huu.
Kiungo huyo, atakumbukwa kwa kufunga
mara zote mbili kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe inayowakutanisha Simba na
Yanga mwaka 2013 na 2014.
Kocha
Mkuu wa timu hiyo Muingereza, Dylan Kerr alisema kiungo huyo amemaliza mkataba
wa kuichezea Simba, lakini ametoa pendekezo la kuongezewa mkataba mwingine.
Kerr alisema, kiungo huyo ni kati ya
viungo bora na kutegemewa kwenye kikosi chake kutokana na uwezo wake wa
kuchezesha na kutuliza timu kwa kukaa na mpira na kupiga pasi safi.
“Kama siyo majukumu ya timu ya
taifa ya Zanzibar Heroes, basi Awadhi angekuwa tayari ameongeza mkataba wa
kuendelea kubaki kuichezea Simba kwenye vipindi vijavyo.
“Lakini mara baada ya kurejea nchini
akitokea Ethiopia kwenye michuano ya Chalenji wanayoshiriki Zanzibar Heroes
atasaini mkataba mwingine kwani bado namuhitaji kikosini,” alisema Kerr.
0 COMMENTS:
Post a Comment