Pamoja na kufunga bao moja tu tangu msimu huu uanze,
straika wa Mtibwa Sugar, Said Bahanuzi, amejipanga kurudisha makali yake ya
kucheka na nyavu mara tu Ligi Kuu Bara itakapoendelea Desemba 12, mwaka huu.
Mtibwa Sugar ambayo inashika nafasi ya tatu katika
msimamo wa ligi ikiwa na pointi 22, imecheza michezo tisa huku ikibakiwa na
michezo sita kuhitimisha mzunguko wa kwanza.
Bahanuzi amesema kuwa
kila kitu kinakuja kwa wakati hivyo amejipanga vizuri kuhakikisha anafunga
mabao ya kutosha katika michezo iliyobakia.
“Unajua suala la ufungaji kwa mchezaji ni kitu cha
kawaida kwa sababu linaongeza changamoto ya kuisadia timu ila jambo la
msingi kwa sasa ni kujipanga na kufanya mazoezi kwa bidii maana
naamini kila kitu kinawezekana, siwezi kukata tamaa.
“Kitu cha kwanza ambacho ni muhimu kwangu ni lazima
nijitoe kwa nguvu zote kuhakikisha naisaidia timu yangu inafanya vizuri katika
mechi sita zilizobaki kabla ya mzunguko wa pili haujaanza kwani itakuwa rahisi
sana kwangu kutimiza kile ambacho nimepanga kukifanya msimu huu,” alisema
Bahanuzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment