November 10, 2015

UHURU SELEMANI AKIZUNGUMZA NA FARID MUSSA ALIPOTEMBELEA KAMBI YA TAIFA STARS KWENYE HOTELI YA HOLIDAY INN EXPRESS JIJINI JOHANNESBURG.
Kiungo mshambuliaji wa Royal Eagles ya Afrika Kusini, Uhuru Selemani amesafiri kilomita 568 kutoka jiji la Durban hadi Johannesburg nchini Afrika Afrika Kusini, kwa ajili ya kuwaona na kuwasalimia wachezaji wa Taifa Stars walio kambini.


Taifa Stars imeweka kambi jijini Johannesburg kujiandaa na mechi dhidi ya Algeria kuwania kucheza Kombe la Dunia ambayo itapigwa Novemba 14 jijini Dar es Salaam.
 

Baada ya kuwasili katika kambi ya Stars, Uhuru alionekana ni mwenye furaha, aliungana na wachezaji, makocha na memba wengine wa benchi la ufundi la Stars.

Alikula nao pamoja na kuzungumza nao hali iliyoonyesha kuchangamsha kambi.
 

“Nilitaka kuja mapema, lakini nisingeweza kwa kuwa tulikuwa tuna mechi ya ligi jana. Tumecheza na kushinda nashukuru.
“Nikaona leo ni siku nzuri kuja kukutana na ndugu zangu. Nimejiona kama niko nyumbani.

“Kweli ni mbali sana, lakini ilikuwa ni lazima nije na kuwaunga mkono ndugu zangu hapa ambao wameweka kambi kulipigania taifa,” alisema Uhuru.

Uhuru aliyewahi kuzichezea Simba, Coastal Union, Mtibwa Sugar na Azam FC, anatarajia kurejea Durban kesho baada ya kukata kiu yake ya kuwaona wachezaji wa Stars, wengi wao akiwa amewahi kucheza nao katika timu mbalimbali.












0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic