November 15, 2015


Nahodha wa timu ya taifa ya Sweden, Zlatan Ibrahimovic amesema ana nafasi ya kuendelea kung’ara kwa kufunga na kutengeneza amabao zaidi.


Zlatan ambaye aliifungia Sweden katika mechi waliyoshinda mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao wakubwa Denmark katika kuwania kufuzu michuano ya Euro amesema ana nafasi ya kuendelea kufanya hivyo kwa kuwa uwezo anao.

“Nina uwezo wa kufanya vizuri, kufunga na kutengeneza mabao kwa zaidi ya miaka mingine mitatu hadi mitano.

“Kweli umri unakwenda, lakini haujamaliza uwezo wangu wote. Ninaweza kuendelea kufunga zaidi, pia kutengeneza zaidi,” alisema Zlatan.


Zlatan anaonekana ndiye mshambuliaji hatari zaidi katika kipindi cha miaka 15 katika kikosi cha Sweden.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic