Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich ametua katika mazoezi ya timu hiyo kwa kushitukiza.
Mfumo huo wa kushitukiza ni kama ule unaotumiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, John Pombe Magufuli kuvamia sehemu ambayo anaona inahitaji marekebisho.
Abramovich, milionea kutokea nchini Russia ametua katika mazoezi ya Chelsea yaliyo katika eneo la Cobham na kuzungumza na wachezaji huku akiwaambia hakuwa akitaka kumfukuza Kocha Jose Mourinho, lakini mwisho haikuwa na namna.
Hata hivyo amewaeleza wachezaji hao kwamba huu ni wakati wa kubadilisha mambo na kusaidia timu kurejea katika hali yake.
Abramovich alizungumza kwa lugha ya Kirusi huku wachezaji wakiatafsiriwa alichokuwa akikieleza.
Mazoezi hayo yalikuwa yakiongozwa na Kocha Steve Holland na Eddie Newton ikiwa ni kujiandaa kwa ajili ya mechi dhidi ya Sunderland kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, Jumamosi.
Taarifa za uhakika kwamba Guus Hidink atakuwa kazini lakini ataanza kwa kukaa jukwaani Jumamosi ili kukiona kikosi hicho kikipambana na Sunderland.
0 COMMENTS:
Post a Comment