December 31, 2015


Zimebaki siku nane kabla ya nahodha wa Yanga, Nadir Haroub Cannavaro kuanza mazoezi mepesi.

Cannavaro amefungwa bandeji ngumu maarufu kama Pop kutokana na mfupa wake mmoja kuwa na matatizo.

“Nadir kaniambia bado kama wiki moja na siku moja hivi ataanza mazoezi mepesi. Lakini hata baada ya kutolewa Pop, atasikilizia kwanza kuona hali yake iko sawa kweli,” alieleza rafiki yake wa karibu.

Cannavaro alitakiwa kukaa nje kwa wiki tatu, yaani siku 21 kutokana na kuwa na majeruhi.

Hata hivyo, daktari wa Yanga, Nassor Matuzya awali alisema ni suala la kuangalia kulingana na maendeleo ya uponaji.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic