Kipa mpya mkongwe wa Azam FC, Ivo
Mapunda, amepanga kutumia michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (Caf) kwa
ajili ya kujitangaza kimataifa ili apate nafasi ya kucheza soka la kulipwa.
Mkongwe huyo, alijiunga na Azam FC
kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu wa Ligi Kuu Bara akitokea Simba
inayoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.
Ujio wake kipa huyo kwenye kikosi cha
Muingereza, Stewart Hall, utaongeza ushindani kwa makipa wa timu hiyo
aliowakuta ambao ni Aishi Manula na Mwadini Ally.
Ivo amesema kuwa ana misimu miwili
hajacheza michuano ya kimataifa akiwa Simba, hivyo amepanga kuitumia kwa ajili
kujitengenezea soka kwenye klabu za nje ya nchi.
Ivo alisema, michuano hiyo inashirikisha
klabu kubwa hivyo anaamini kama akiitumia vizuri, basi kuna uwezekano wa kupata
dili la kwenda kucheza nje ya nchi kutokana na uwezo wake mkubwa alionao wa
kuokoa michomo golini.
Aliongeza kuwa, katika hilo, anaamini
atafanikiwa kutokana na safu bora ya ulinzi iliyopo Azam ikiongozwa na Muivory
Coast, Pascal Wawa na Aggrey Morris.
“Azam nataka kuitumia kama njia ya
kujitengezea soko la kucheza soka la kimataifa kutokana na ushiriki wa michuano
ya kimataifa tutakayoshiriki, mwakani.
“Ninajua haitakuwa rahisi kwangu
kujitengenezea soko la kucheza soka la kimataifa bila ya bidii na kujituma
kwangu ndani ya uwanja, hivyo napanga kuitumia michuano hiyo kujitangaza,”
alisema Ivo.
0 COMMENTS:
Post a Comment