December 30, 2015




Kampuni ya Alkamistr Media inayojishughulisha na uandaaji wa filamu nchini,  usiku wa kuamkia leo ilizindua filamu mpya inayokwenda kwa jina la Homecoming.

Sasa filamu hiyo na nyingine zinaonekana kwenye Chaneli ya Sinema Zetu na sasa ni kwenye Golden Premiere ndani ya king'amuzi maarufu na bomba cha Azam TV.


Filamu hiyo iliyochezwa kwa mrengo wa kuelimisha juu ya masuala ya kutokomeza ufisadi mbalimbali, ilizinduliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye,  ndani ya ukumbi wa kuonyeshea sinema uliopo katika jengo la Mlimani City jijini Dar es Salaam.  

Akizungumza muda mfupi kabla ya uzinduzi huo kufanyika Nape alisema kuwa anawashukuru waandaaji wa filamu hiyo kwa kumpatia fursa ya pekee kwa ajili ya kuizindua filamu hiyo ikiwa ni moja ya mwendelezo wa kuthamini kazi za wasanii mbalimbali hapa nchini.


“Nimefarijika sana kuona leo tumekusanyika kwenye ukumbi huu kwa ajili ya kuzindua filamu ya Kitanzania, hivyo niwapongeze wamiliki wa ukumbi huu kwa kuruhusu kuonyeshwa kwa filamu hii hapa, najua ni mwanzo na itakuwa faraja zaidi siku nyingine nikija hapa nikute filamu  zetu zikionyeshwa maana najua huwa ni adimu mno kuona sehemu kama hii watu wameketi kuangalia filamu zetu..


“Kufanya hivi mimi nina imani kuwa ni njia mojawapo ya kukuza soko letu ambalo tunajitahidi kupambana ili tuweze kutokomeza wizi huku tukinyanyua ajira kwenye sanaa hii,” alisema Nape.










0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic