Pamoja na meneja wake, Jamal Kisongo kusema tayari Mbwana Samatta amesaini mkataba wa awali wa miaka miwili na Genk, mshambuliaji huyo amesema bado wanaendelea kuwasubiri TP Mazembe.
“Bado tunasubiri Genk wamalizane na Mazembe, huwezi kumsainisha mchezaji wa timu nyingine mkataba. Lakini mimi nimeshamalizana na Genk kwa maana ya makuabaliano, suala la mkataba litafuatia,” alisema Samatta.
Samatta anatarajia kuondoka nchini kwenda Nigeria katika tuzo za mchezaji bora wa Afrika yeye akiwa anawania tuzo ya wachezaji wanaocheza ndani ya bara la Afrika.
Samatta anapewa nafasi ya kutwaa tuzo hiyo kutokana na kuisaidia TP Mazembe kutwaa ubingwa wa Afrika pamoja na yeye kuibuka mfungaji bora.
Tamasha maalum la tuzo hizo limepangwa kufanyika Januari 7 jijini Lagos, Nigeria ikiwa ni siku mbili tu baada ya Samatta kutua nchini humo.
0 COMMENTS:
Post a Comment