December 7, 2015

KIMWAGA (KATIKATI) AKISHANGILIA NA WENZAKE BAADA YA KUIFUNGIA SIMBA BAO.

Kiungo wa Simba, Joseph Kimwaga, amezuiwa kucheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC itakayopigwa Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Kimwaga anaichezea Simba kwa mkopo akitokea Azam na kilichosababisha azuiwe ni kuwa katika taratibu walizojiwekea Azam, ni kuwa wachezaji wao wote waliowatoa kwa mkopo hawaruhusiwi kucheza dhidi ya Azam FC.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, alisema kuwa Kocha wa Simba, Dylan Kerr, akae akijua kabisa kuwa mchezaji huyo hatamtumia katika mchezo huo.

 “Inafahamika kuwa Kimwaga yupo Simba kwa mkopo, hivyo bado ana mkataba na Azam, kwa hiyo anahesabika ni mchezaji wetu.

“Sisi taratibu zetu zipo hivi, hatuwaruhusu wachezaji tuliowatoa kwa mkopo kuchezea timu zao walizopo pale tunapokutana nazo, hivyo Kimwaga hataichezea Simba Jumamosi,” alisema Kawemba

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic