December 26, 2015




MPIRA UMEKWISHAAA
Dakika 3 za nyongeza
Dk 89, Lyanga anapata pasi nzuri kabisa, lakini mwamuzi anasema ameotea
SUB Dk 85 Fabian Gwanse anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Julius Mrope

GOOOOOOOOO Dk 85, krosi safi ya Kazimoto, Brian Majegwa anafunga vizuri kabisa
Dk 84, Yanga anapata nafasi nzuri lakini anashindwa kuwa makini

GOOOOOOOO Dk 76, Nizar Khalfan anafunga bao zuri kwa kisigino akiunganisha kona safi kabisa iliyochongwa. Alipiga huku mabeki wa Simba wakiwa wamzubaaa

SUB Dk 72, Kiiza anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Kiongera
Dk 69 Jabir Aziz anapiga krosi nzuri lakini Juuko anawahi na kuokoa
Dk 66 Ajib anapiga krosi lakini Mgeveke anaondosha vizuri kabisa katika eneo la hatari

KADI Dk 61, Jabir Aziz analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Ajib
SUB Dk 59, Brian Majegwa anaingia kuchukua nafasi ya Said Ndemla

Dk 58, Lyanga anajaribu kwa mara nyingine, anapiga shuti lakini Kado anadaka vizuri
Dk 51 Mnyate anaingia vizuri lakini Juuko anamuangusha, mwamuzi anamuita na kumuonya, faulo inapigwa lakini haina madhara

Dk 47 Simba wanaanza kwa kushambulia wakilisakama lango la Mwadui ingawa bado hawajapata dawa ya kuipenya ngome na kumfikia Kado
MAPUMZIKO
+2 (Dakika mbili za nyongeza)
Dk 45, Mnyate anapiga krosi nzuri lakini Agbani anawahi na kudaka
Dk 43, Lyanga anapiga shuti kali lakini lipaaa juuuu

Dk 40 hadi 42, mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja huku Simba wakimiliki zaidi mpira lakini wanashindwa kumalizia kila wanapofika langoni mwa Mwadui
Dk 39, Mkude tena anapiga shuti kali lakini linakuwa "bonge la mnazi"
Dk 37, Tshabalala anapiga krosi safi lakini Ndeule anaokoa na kuwa kona ya kwanza ya mchezo huu, kona nzuri kabisa inachongwa Kiiza anapiga kichwa safi lakini hakulenga

Dk 32, Kessy anamuangusha Mnyate katika eneo nje kidogo ya 18, mwamuzi anasema ipigwe faulo, MWadui Nizar Khalfan anachonga lakini nje
Dk 26, Lyanga anajaribu kupiga shuti, hata hivyo linakuwa si kali Kado anadaka vizuri

Dk 20, Tegete anapiga shuti lakini Agban anadaka kama nyani

Dk 19 Tshabalala anaokoa mpira wa kichwa kabla haujamfikia Malika Ndeule
Dk 16, Kado anafanya kazi ya ziada kupangua mpira wa Tshabalala na kuwa wa kurusha
Dk 13, Kiiza anaubetua na kupiga shuti kali lakini anapaisha juuu

Dk 9, Kessy tena anapokea pasi nzuri ya Ndemla, anajaribu kupiga krosi anajichanganya na kuwa goal kick
Dk 5, Kessy anaingia vizuri lakini mwisho naye anashindwa kupiga krosi, anautoa mpira unatoa goal kick

Dk ya kwanza hadi ya nne, timu zinaonekana kucheza mpira zaidi katikati ya uwanja kama zinaibiana, lakini hakuna mashambulizi makali

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic