Kiungo mwenye kasi wa Yanga, Simon Msuva ameshindwa kwenda kazini leo na kulazimika kutokana na kubanwa na malaria.
Msuva ameshindwa kwenda mazoezini wakati Yanga ikijifua kwenye Uwanja wa Boko jijini Dar es Salaam, leo.
Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh ameiambia SALEHJEMBE kwamba Msuva ameshindwa kwenda mazoezini kutokana na malaria.
Lakini baadaye Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema kuwa amepata taarifa hizo za ugonjwa na kumtakia heri Msuva apone haraka.
"Tumeendelea na mazoezi vizuri, lakini Msuva pia tumemkosa kwa kuwa anaumwa malaria. Akipona, tutaungana naye kwa ajili ya mapambano," alisema Pluijm.
0 COMMENTS:
Post a Comment