Na Maulid Kitenge
MOHAMED DEWJI Mo bilionea anayetaka kuwekeza bilioni 20 ameupa uongozi wa Simba hadi keshokutwa Desemba 31 wawe wameamua moja juu ya kukubali au la mpango wake wa kufanya uwekezaji wa kiasi hicho cha fedha kwa nia ya kuiendesha klabu hiyo kibiashara.
DEWJI Mo ameniambia E. sports ya E FM katika mahojiano maalum leo asubuhi ofisini kwake kuwa anataka viongozi wa Simba chini ya Rais Evans Aveva waamue moja kama wako tayari Au la na ikifika keshokutwa kama hawatafanya maamuzi yeye hatoendelea tena na mpango huo na badala yake ataendelea na biashara zake
MOHAMED DEWJI Mo anataka kuwekeza kiasi cha sh. Bilioni 20 kunako klabu hiyo kwa nia ya kuiendesha kibiashara klabu hiyo kongwe kabisa barani Afrika.
Anasema alikutana na viongozi wa SIMBA Rais Evans AVEVA, akiwa na KASSIM DEWJI na Musley Ruhwehi ofisni kwake na kuwaeleza dhamira yake hiyo lakini anaona viongozi hao kama hawako tayari kwa sasa kuona klabu hiyo inaendeshwa kibiashara kwani mpaka sasa hawajampa jibu la kueleweka.
"KITENGE nakutuma kawaambie wana Simba kwa ujumla kuwa nimewapa viongozi wao mpaka Desemba 31 kama hawatafanya maamuzi ya hilo basi nafuta mpango huo na wasinitafute tena Maana hawatanipata na cm zao sitopokea. Amesema MOHAMED DEWJI Mo ambaye anatajwa kuwa tajiri zaidi Kijana nchini Tanzania.
Mo anasema chini ya uwekezaji atakaofanya atajenga Kiwanja cha Bunju na kuwa Kiwanja maalum cha mazoezi ya klabu hiyo na pia kama kituo maalum cha kulea vipaji vya soka kwa vijana ambao baadaye watachezea timu hiyo ya SIMBA.
Mo amesema mipango yote hiyo tayari amewaeleza viongozi wa SIMBA chini ya Rais AVEVA lakini akashangaa mpaka sasa viongozi hao wamekuwa hawanyooshi maneno na badala yake wanasema bado hawajapata barua rasmi kutoka kwake.
Anasema tumeongea hapa ofisini kwangu na viongozi na kuwaeleza ambapo pia nimewaambia tutaunda bodi ambayo itakuwa na watu saba wanne watatoka kwake Mo na watatu watatoka upande wao wa uongozi kwa nia ya kuendesha kibiashara.
Mo anasema anataka mpango huo uanze haraka iwezekanavyo ikibidi Januari ili kuanza pia mchakato wa kutuma mascout kusaka wachezaji watakaochezea Simba baada ya kumalizika kwa Ligi hii inayoendelea.
Hii ni nafasi ambayo Simba tukiipoteza tutajuta kwa miaka mingi sana.... Na moja ya sababu inayoweza kunistaafisha kuishabikia kwa nguvu timu yangu ya Simba na soka la bongo ni hii
ReplyDeleteUkweli watu waliozoea kudokoa ndio wanalimaliza soka la bongo,maana wanajua MO akichukua timu wao hawana chao ndio maana wanasuasua kulitolea maamuzi jambo hilo.
ReplyDeletePropperties Turstees wa club ya simba ni Baraza la Wadhamini hivyo MO alitakiwa kujadiliana na Baraza na si uongozi ambao wenyewe mandate yake ni kutafuta ventures za investment tu
ReplyDelete