Mshambuliaji nyota wa Yanga, Amissi Tambwe ameshindwa kufanya mazoezi leo kutokana na maumivu ya mkono yaliyotokana na kuanguka.
Tambwe alianguka baada ya kufunga bao la kwanza wakati Yanga ilipoivaa Mbeya City na kushinda kwa mabao 3-0 yeye akiwa amefunga matatu.
Katika mazoezi ya Yanga leo kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Tambwe alikaa nje na kuwaangalia wenzake wakijifua.
Hata hivyo alipatiwa matibabu ili kuendelea kuupoza uvimbe huo.
"Saa hizi naona umepungua ukilinganisha na siku ile baada ya mechi. Unajua niliporuka kupiga mpira baada ya kuutuliza kifuani, niliumia," alisema Tambwe.
0 COMMENTS:
Post a Comment