January 26, 2016



Emmanuel Adebayor amesaini mkataba wa miezi 18 na Crystal Palace.

Imeelezwa mkataba huo unatakiwa kuish mwisho wa msimu huu lakini utakuwa na vipindi kama pande mbili zitakubaliana kuongeza.


Palace inayonolewa na Allan Pardew itakuwa ikimlipa mshahara wa pauni 70,000 kwa wiki, huku timu yake ya Tottenham ambayo mkataba haujaisha itakuwa inalipa pauni 30,000 kwa wiki ili kukamilisha malipo ya pauni 100,000 kwa wiki anayotakiwa kupata.



Mshambuliaji huyo mwenye miaka 31, raia wa Togo aliendelea kubaki kwa huku akisubiri dirisha dogo lifunguliwe.

Lakini wakati huo Spurs iliendelea kumlipa pauni 100,000 kwa wiki kama mkataba wake ulivyokuwa ukisema.

Mkataba wake na Spurs unaisha Juni, mwaka huu lakini klabu hiyo inatakiwa kuendelea kumlipa hadi Septemba, mwaka huu.

Baada ya Arsenal, Manchester City na Spurs, Adebayor anaichezea Palace kama klabu yake ya nne katika Ligi Kuu England.


Pia amewahi kukipiga katika klabu ya Real Madrid iliyokuwa chini ya Jose Mourinho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic