January 26, 2016

MATOLA

 Geita Gold Sports imeonyesha hata timu ya daraja la kwanza inaweza kuitoa ya Ligi Kuu baada ya kuitwanga Mgambo JKT kwa penalti 4-3 katika mechi ya Kombe la FA linalodhaminiwa na Azam Sports.

Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sekondari ya Wanawake ya Nyankumbu na Geita Gold Sports inayofundishwa na Selemani Matola imetinga hatua ya 16 Bora ya Kombe la FA.

Kusonga hatua ya 16 Bora, maana yake kikosi cha Matola kinaungana na Simba, Yanga na Azam FC ambazo zimeshafuzu hatua hiyo.

Geita Gold inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, ilianza kufungwa dakika ya 14 kwa bao lililofungwa na Bolly Shaibu dakika ya 20 baada ya kupokea pasi ya Salim Gilla.

Zikiwa zimebaki dakika nne kwenda mapumziko, Geita ilipata penalti na kusawazisha bao hilo mfungaji akiwa ni Omary Kanyoro na kwenda mapumziko timu hizo zikiwa sawa kwa bao 1-1.

Hata ziliporudi kipindi cha pili zilishambuliana kwa zamu lakini hakuna timu iliyoweza kupata bao ndipo mwamuzi alipoamuru kupigwa mikwaju ya penalti ili kupata mshindi.


Geita ilifanikiwa kupata penalti nne dhidi ya tatu za Mgambo inayoshiriki Ligi Kuu Bara na kutinga 16 Bora ya Kombe la FA na sasa inasubiri kucheza mechi nyingine za michuano hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic