January 26, 2016



Beki mkongwe wa Yanga, Kelvin Yondani amesema ugumu wa Ligi Kuu Bara unazidi kuongezeka kadiri ligi hiyo inavyosonga mbele.

Yondani ambaye amekulia kisoka mkoani Mwanza amesema ligi hiyo imekuwa ikizidi kuwa ngumu kwa kuwa kila timu inajitahidi kutokosea.

“Si rahisi kupima timu fulani imefungwa na timu fulani, basi mkikutana nayo itafungika kwa ulaini, ligi ni ngumu sana.

“Hauwezi kuwa na uhakika wa ushindi hadi mwisho, utaona kikosi chetu ni bora. Lakini kuna wakati tunapambana sana ili kushinda,” alisema.


Yondani amekuwa katika kiwango kizuri katika kipindi hiki hali iliyosababisha awe msaada mkubwa kwa safu ya ulinzi ya Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic