Mtibwa Sugar imefanikiwa kuongeza pointi 3 za Ligi Kuu Bara baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stand United kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani.
Dakika 45 za mechi hiyo zimechezwa leo baada ya jana kuchezwa kipindi kimoja na mechi kuahirishwa kutokana na mvua kubwa.
Bao lilifungwa na Muzamiru Yassin akiunganisha mpira wa kona wa Shiza Kichuya. Hadi mechi inaahirishwa Mtibwa ilikuwa mbele kwa bao hilo moja.
Kipindi kimoja cha leo, hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao na Mtibwa Sugar kutoka uwanja na pointi hizo tatu zinazoifanya kufikisha pointi 31 katika nafasi ya nne, nyuma ya Yanga, Azam FC na Simba.








0 COMMENTS:
Post a Comment