NUHU (KUSHOTO) SIKU ALIPOSAINI SIMBA... |
Aliyekuwa beki wa Simba, Samih Haji Nuhu ambaye kwa sasa anamilikiwa na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Zanzibar, Mafunzo, amesema kuondoka kwake Simba kulitokana na uongozi kutomjali.
Samih amesema hakuondoka Simba kwa kufukuzwa lakini kikubwa ni uongozi kutomtimizia mahitaji yake, madai ambayo yanafanana na yaliyotolewa hivi karibuni na kiungo wa timu hiyo, Justice Majabvi, lakini alielewana na uongozi wake baada ya muda na sasa mambo ni mazuri.
"Uongozi hauangalii nini mchezaji afanyiwe, kwa sababu wanaingilia mambo ya makocha, viongozi hawakuwa wakitenda haki kwa wote, mimi nimeondoka kwa nia nzuri, ili siku nyingine wakinihitaji nirudi kwa amani,” alisema beki huyo na kuongeza:
“Mfano kama hata (Elias) Maguri aliondoka Simba kutokana ya viongozi kutokuwa makini kwenye kazi yao na hawafai hata kuwepo klabuni hapo.”
0 COMMENTS:
Post a Comment