January 1, 2016


Baada ya bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka ‘SMG’ kuchezea kichapo kutoka kwa Thomas Mashali ‘Simba Asiyefugika’, baba mzazi wa bondia huyo, Boniphace Cheka ameibuka na kusema sababu kubwa ya mtoto wake kupigwa ni baada ya kupuuza masharti ya mizimu.

Katika pambano hilo la raundi 10 lililofanyika wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Cheka alipoteza kwa pointi 96-99, 93-96, 93-97 na hivyo kuvunjwa kwa rekodi yake ya kutopigwa kwa muda wa miaka 12 na mabondia wa Tanzania.

“Unajua nilishawahi kusema kwamba mwanangu  hatapigwa katika kipindi chote ambacho nitakuwepo hapa duniani kwa sababu siku zote nimekuwa nikiomba kwa mizimu iweze kumlinda kabla ya kupanda ulingoni.

“Kiukweli nilimwambia aje nimuombee siku moja kabla ya kupima uzito ili aweze kushinda, lakini cha kushangaza hakuweza kufika na ndiyo maana alipigwa kwa sababu amevunja masharti ya mizimu yangu na siyo kwa uwezo wa huyo aliyempiga,” alisema Mzee Cheka.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic