January 25, 2016


Beki wa zamani wa Simba, Emily Mugeta amefanya mazoezi ya ngumi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Ligi Daraja la Tano nchini Ujerumani.

Mgeta anakipiga katika klabu ya daraja la tano ya Neckarsulmer, amesema wamefanya mazoezi hayo ikiwa ni sehemu ya kuongeza uimara na wepesi.

"Kila kitu ni mafunzo, sikujua kama unaweza kucheza ngumi katika soka, lakini yalikuwa mazoezi mazuri na nimepata kitu kipya," alisema Mgeta.

Mgeta aliyewahi kukipiga Simba akianzia katika timu ya vijana, yuko katika harakati za kurejesha kiwango chake baada ya kuwa amerejea Tanzania baada ya kufiwa na ndugu yake.

KUMRADHI, AWALI HABARI HII ILIKOSEWA NA KUCHANGANYWA NA ILE YA MWANASHERIA WA YANGA.











2 COMMENTS:

  1. Hahahahahahhaahah!haki ya nani mweee!
    imebidi tu nicheke mengine angalia mwenyewe tatizo liko wapi.

    ReplyDelete
  2. Muwe makini wakati mnarusha habari. Maelezo ya habari ya Emily mgeta haina uhusiano na masuala ya mwanasheria wa yanga kuachishwa kazi. Mhariri mkuu bwana saleh tunaomba uwemakini na uzingatie weledi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic