January 25, 2016

MADEE

Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Hamad Ally ‘Madee’ amefunguka katika mahojiano na SALEHJEMBE kuhusiana na sakata lake la kwamba kama Arsenal ambayo anaishabikia, ingefungwa na Chelsea, basi angelichoma moto gari lake aina ya Lexus.

Picha zilizagaa mitandaoni jana mchana zikionyesha Madee akiwa na ufunguo mkononi, akionyesha gari hilo kwamba angelitia kibiriti kama Arsenal ingepoteza mechi hiyo ya Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea jana.

Mechi ilimalizika kwa Chelsea kuituliza Arsenal kwa bao 1-0, baada ya hapo wanahabari na mashabiki walianza kumsaka Madee ili achome moto gari hilo baada ya Arsenal kulala.

“Kweli nimepigiwa simu nyingi sana, jamaa wamenitafuta mno. Lakini ukweli nilisema kama sehemu ya mzaha wa kuongeza chachu na utani wa kimichezo.

“Sikuwa nikimaanisha, lakini naona hata comment ni nyingi mni kwenye ukurasa wangu wa Instagram,” alisema na alipoulizwa taarifa kwamba leo asubuhi alikuwa analichoma gari hilo na picha zinaonekana mtandanoni.

“Siwezi kufanya upuuzi huo brother, hao wanaosema hivyo nafikiri wanataka kupata followers kwa ujanja mwingine. Naendelea kusisitiza ule ulikuwa ni utani wa kimichezo. Mimi napenda soka na nilfanya vile kama kuchangamsha tu,” alisema Madee maarufu kama Rais wa Manzese jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic