January 25, 2016


 Yanga sasa inapaa kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kujiweka vizuri na Ligi ya Mabingwa Afrika.
 Lengo la Yanga ni kupata mechi kadhaa za kirafiki ili kujiweka fiti zaidi na Kocha hans van der Pluijm atapata muda wa kutosha wa maandalizi.
 Mkuu wa Kitengo cha habari cha Yanga, Jerry Muro amesema wataondoka nchini Ijumaa kwa ajili ya kambi hiyo.
“Tuko katika maandalizi ya mwisho kwa ajili ya kutafuta mechi za kirafiki ambazo zitatusaidia kuwa fiti zaidi.
 “Mnajua ugumu wa michuano ya kimataifa, sisi ni wa kimataifa na maandalizi yetu lazima yawe ya kimataifa,” alijigamba Muro.

Kambi ya Yanga inatarajia kuwa katika mji wa Johannesburg ambako itaweka kambi inayotarajiwa kuwa ya zaidi ya siku tano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic