January 25, 2016

MAXIME

Kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime, amesema hivi sasa  Tambwe ndiye mshambuliaji mwenye thamani kubwa kushinda wengine wote wanaoshiriki ligi kuu, wakiwemo Kipre Tchetche wa Azam na Hamis Kiiza wa Simba.

“Kama wakiniambia kuwa ni mshambuliaji gani ambaye kwa sasa ningependa kuwa naye katika kikosi changu, basi nitasema ni Tambwe kwa sababu anajua majukumu yake uwanjani kuliko washambuliaji wengine.

TAMBWE


“Siku zote kazi ya mshambuliaji ni kufunga, achana na mbwembwe nyingine, hivyo Tambwe ni namba moja kwangu kwa washambuliaji na kama ningekuwa naye katika kikosi changu, hakika tungetisha sana kwani nina viungo bora kabisa ambao angeshirikiana nao kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,” alisema Maxime.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic