BOSSOU |
Beki wa kimataifa wa Yanga, Vincent Bossou ametamba kuwa hata nahodha wa kikosi hicho, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ atakaporejea atahakikisha yeye anaendelea kucheza ndani ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Bossou ambaye awali hakuwa na namba, amekuwa tegemeo kwenye safu ya ulinzi ya timu hiyo tangu Cannavaro apate majeraha ya mfupa wa kisigino ambayo yatamfanya akae nje ya uwanja kwa miezi kadhaa.
Bossou alisema kuwa yupo kwenye kiwango kizuri na anataka kuendelea kuonyesha kiwango zaidi ili kuzidi kujihakikishia namba ndani ya kikosi hicho na hatataka kuipoteza kirahisi nafasi hiyo hata pale Cannavaro mwenye namba yake atakaporejea kikosini.
CANNAVARO |
“Kelele za mashabiki wakati ule nilipokuwa ninakaa benchi zilikuwa zikiniumiza sana kwani wengi wao walikuwa hawajui nini ambacho nilikuwa ninakifanya, kwanza nilikuwa mgeni na nisingeweza kuharibu kikosi nilichokikuta kwa urahisi.
“Lakini sasa nimepata namba ya kuanza na nitahakikisha ninapigana kwa uwezo wangu wote kuhakikisha ninailinda namba hii hata pale Cannavaro atakapopona,” alisema Bossou.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment