January 9, 2016


Kama ulidhani nahodha na beki wa kati wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ anaona poa jinsi Vincent Bossou anavyocheza kwenye nafasi yake sahau kuhusu hilo. 

Cannavaro amesema kuwa, anarejea uwanjani muda siyo muda mrefu, hivyo Bossou ajiandae kumpisha katika nafasi yake.

Nahodha huyo yupo nje ya uwanja kwa wiki mbili sasa akiuguza majeraha ya enka kwenye mguu wake wa kulia alioumia katika mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Etoile du Sahel kabla ya kujitonyesha na kuwekewa bandeji ngumu yaani P.O.P hivi karibuni.

“Kati ya vitu ambavyo sivifikirii kabisa ni kukaa benchi mara nitakaporejea uwanjani baada ya kupona majeraha yangu ya goti, naamini nina uwezo mkubwa na nitacheza.

“Kila mtu anajua kuhusu uwezo wangu, iweje nihofie kuhusu kucheza? Najua wapo wachezaji wengine wenye uwezo wa kucheza nafasi hiyo, lakini nikirudi narudi moja kwa moja kwenye nafasi yangu,” alisema Cannavaro.

Katika mechi za Kombe la Mapinduzi huko Zanzibar, Bossou anacheza nafasi ya Cannavaro sambamba na Kelvin Yondani licha ya awali nafasi hiyo kuchezwa na Pato Ngonyani.


Yanga ipo Kundi B na kesho Jumapili itacheza mechi yake ya nusu fainali ya michuano hiyo inayochezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic