NONGA |
Yanga ina zaidi ya washambuliaji watano kwa sasa ila wanaotazamwa kwa sana ni Donald Ngoma raia wa Zimbabwe na Amissi Tambwe wa Burundi.
Lakini huo ni mtego kwani Yanga ina mastraika wengine wawili wazawa, Paul Nonga na Malimi Busungu, hao jamaa ni hatari na wote wameshafunga bao moja moja kwenye Kombe la Mapinduzi wakitokea benchi.
Huwa wanaingia kutoka benchi na wakiwa huko kazi yao huwa kusoma makosa ya wapinzani na wakiingia huonyesha uhai wakicheza sambamba.
NONGA |
Nonga aliyejiunga na Yanga Desemba mwaka jana akitokea Mwadui FC, alifunga bao moja dhidi ya Mafunzo akitokea benchi na Busungu alifunga dhidi ya Mtibwa Sugar pia akitokea benchi.
Kocha wao, Hans van Der Pluijm raia wa Uholanzi amebaki mdomo na kutoamini jinsi Nonga na Busungu wanavyofanya vizuri uwanjani.
Pluijm alisema kuwa hali hiyo inamfanya awe na amani zaidi kwani hata kama Ngoma na Tambwe wasipokuwepo ana watu ambao wanaweza kumpatia matokeo mazuri.
“Hakika Busungu na Nonga wamefanya kile ninachokita, nawaomba wazidi kujituma zaidi ya hapo, kwani pacha yao nimeikubali na nitaendelea kuwatumia kama ninavyofanya siku zote.
“Niliamua kuwapa nafasi ya kuwachezesha pamoja baada ya kuona kuwa Ngoma na Tambwe wamechoka na wanahitaji kupumzika, lakini kazi yao nimeibukabili,” alisema Pluijm.
0 COMMENTS:
Post a Comment