January 2, 2016

FARID
Kiungo mwenye kasi wa Azam FC, Farid Mussa hayupo katika kikosi cha timu hiyo kitakachocheza mechi za Kombe la Mapinduzi kuanzia kesho Jumapili badala yake wiki ijayo atakwenda kufanya majaribio nchini Slovenia.

Farid atakwenda kufanya majaribio katika Klabu ya NK Olimpija Ljubljana inayoshiriki ligi kuu nchini Slovenia na mambo yakienda sawa atasajiliwa kuichezea timu hiyo.
Olimpija iliyoanzishwa miaka kumi iliyopita, kwa sasa ipo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu inayojulikana kama Slovenian PrvaLiga ikiwa na pointi 46 baada ya kucheza mechi 22.

Kocha wa Azam, Stewart Hall, amesema nafasi ya Farid katika kikosi chake kwenye Kombe la Mapinduzi itachukuliwa na Gadiel Michael.

“Wiki ijayo Farid anatarajiwa kwenda Slovenia kufanya majaribio katika timu ya Olimpija kwa muda wa wiki moja hadi mbili, hivyo hatutakuwa naye katika Kombe la Mapinduzi.

“Nafasi yake atakuwepo Gadiel, huyu ni mchezaji mzuri anayemudu kufanya kazi za Farid kikosini,” alisema Hall raia wa Uingereza.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic