January 2, 2016


Unaweza kusema taratiiibu kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Ramadhan Singano ‘Messi’ ameanza kuikumbuka timu yake ya zamani ya Simba kutokana na ukweli kwamba sasa hana nafasi kikosi cha kwanza. 

Singano amejiunga na Azam msimu huu, na tangu ajiunge na timu hiyo hajafanikiwa kuifungia bao lolote lakini ametoa pasi mbili za mabao huku akiwa hana nafasi ya kudumu kikosini.  

Singano amesema anashindwa kufunga kutokana na kutopata nafasi ya kucheza mara kwa mara tofauti na alivyokuwa Simba kwa kuwa timu hiyo ina kikosi kipana.

“Watu hawapaswi kunifikiria tofauti kwa sababu hakuna mchezaji asiyependa kufunga hasa akiwa na uwezo wa kufanya hivyo, Azam ni timu kubwa na ina wachezaji wengi tofauti na timu niliyotoka.

“Sasa kila kitu kinahitaji muda ili kiweze kuwa sawa maana huku mara nyingi nachezeshwa namba kumi wakati Simba nilikuwa nikicheza namba 11 ambayo ilikuwa ina faida kwangu.


“Nadhani kila mtu anaona aina ya wachezaji waliopo hapa wana ushindani mkubwa na hakuna mwenye nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza,” alisema Singano. 

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic