January 2, 2016


Simba SC ina mastraika nane ila bado haina makali katika ufungaji, hivyo Kocha Dylan Kerr ameamua kuwatumia viungo wake wakiwemo Said Ndemla na Mwinyi Kazimoto katika upikaji mabao ikiwezekana hata kufunga. 

Mastraika nane wa Simba ni Hamis Kiiza, Paul Kiongera, Danny Lyanga, Ibrahim Ajibu, Hija Ugando, Joseph Kimwaga, Mussa Mgosi na Brian Majwega.
Kerr raia wa Uingereza amesema kuwa, katika kikosi chake anamkosa mtu mmoja tu, naye si mwingine bali ni kiungo mpika mabao.

Kutokana na usajili kufungwa Kerr amedhamiria kukomaa na viungo wake wa sasa ili kutibu tatizo hilo kikosini mwake.

Simba ina viungo saba ambao ni Kazimoto, Ndemla, Justice Majabvi, Jonas Mkude, Awadh Juma, Peter Mwalyanzi na Abdi Banda.

 “Haiwezekani tuwe na mastraika wengi halafu tuhangaike kwenye kufunga mabao, kwa kweli inaniuma na tayari nimeshajua tatizo lilipo.


“Viungo nilionao nitawapa mazoezi maalum ambayo yatakuja kutibu tatizo hilo, na muda si mrefu mabao yataanza kuja,” alisema Kerr.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic