January 7, 2016


Picha hizi tatu zinaonyesha hakukuwa na usalama hasa kati ya wachezaji wawili wote wageni kutoka nje ya Tanzania wakati Yanga na Azam FC zilipocheza mechi yao ya makundi katika michuano ya Mapinduzi mjini Zanzibar, juzi.

Beki wa Azam FC, Sergio Wawa alikuwa wa kwanza kumchapa kofi mshambuliaji Donaldo Ngoma wa Yanga wakati wakibishana.
Wawa raia wa Ivory Coast, alisukuma kofi lililompata Ngoma vizuri. Naye kuona hivyo, hakukubali na kuanza kupambana vilivyo na kwa kumkaba kwa nguvu Wawa aliyeonekana kuchanganyikiwa.

Hata hivyo, Thabani Kamusoko, Dues Kaseke na Ramadhani Singano walishirikiana kufanya kazi ya ziada na kupoza msala huo ambao ulikuwa haishikiki. Angalia picha vizuri.






1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic