Kiungo wa Simba, Ibrahim Ajib pamoja na kuibuka shujaa lakini alijikuta akilambwa kadi ya njano kutokana na uamuzi wake wa kuvua kiatu na kupiga simu.
Ajib ndiye alifunga bao pekee wakati Simba ikiilamba Ndanda FC kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa Nangwana mjini Mtwara.
Mara baada ya Ajib kufunga bao hilo, haraka alikimbia na kuvua kiatu halafu akaigiza kama alikuwa akipiga simu na kuzungumza na mtu.
Mwamuzi hakumuacha, mara baada ya kumaliza kushangilia, akamlamba kadi ya njano fasta huku Ajib akionekana kulalamika.
0 COMMENTS:
Post a Comment