January 16, 2016


Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Nadir Ali Haroub, sasa ameamua kuutumia muda wake mwingi kukaa dukani akimsaidia mkewe.

Cannavaro ameamua kufanya kazi ya kuuza duka kwa kuwa ni majeruhi na alifungwa pandeji ngumu ya Plasta Of Paris maarufu kama POP.

Kwa sasa Cannavaro amekuwa akisakwa na vyombo vya habari wengi wakitaka kupata mwenedelezo wake baada ya ile kauli yake kutoka katika gazeti la Championi, kwamba ameamua kustaafu kuichezea timu ya taifa.

Cannavaro ameamua kustaafu baada ya kuvuliwa unahodha na kupewa Mbwana Samatta, lakini yeye aliona hilo kwenye runinga.


Baada ya hapo, alieleza wazi alivyoumizwa na suala hilo. Akaweka wazi namba ambavyo amekuwa akipokea lawama, lakini kuvuliwa huko unahodha bila utaratibu ndiyo kumemkwaza zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic