January 16, 2016


MPIRA UMEKWISHAAAA
Dk 90, krosi nyingine safi ya Baba Ubaya, Agbani anaruka na kuanguka. Anatibiwa tena, huku wachezaji wa Mtibwa Sugar wakilalama kwamba anapoteza muda
KADI Dk 90 Agbani analambwa kadi ya njano kwa kujiangusha makusudi na kusema alikuwa ameumia
Dk 90 kipa Agbani wa Simba, yuko chini anatibiwa ni baada ya kuutoa mpira nje na kusema aliumia mgongo
Dk 90 Agbani anafanya kazi ya ziada kuokoa krosi ya Kichuya

+4
Dk 90, Mtibwa Sugar wanapata nafasi nzuri lakini Jaffar anashindwa kuitumia kwa kubutua shuti kuuubwaaa
SUB Dk 89 Awadhi Juma anaingia kuchukua nafasi ya Kiiza upande wa Simba
Dk 86, Barbabas ananajribu kumtoka Isihaka, unatokana kuwa kona ya tano. Inachongwa na Baba Ubaya lakini Agbani anakamata.

Dk 82, Kibaya anageuka na kupiga shuti la kushitukiza, mpira unamgonga Isihaka, kona. Inachongwa na Kichuya lakini haina madhara
Dk 79, Mbonde anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira na kuwa kona, inachongwa na Lyanga, kwake Tshabalala, mpira unamfikia Kiiza peke yake lakini anashindwa kutulia, anapiga nje

Dk 78, mabeki Mtibwa Sugar wanachanganyana na kipa wao, lakini Simba wanashindwa kuwa wepesi kuuwahi mpira
Dk 75, Jeba naye anapiga shuti kali lakini mpira unatoka mbali ya lango la Mtibwa Sugar
Dk 74, Kiiza anajaribu kwa kupiga shuti kali tena la kushitukiza, lakini linatoka sentimeta chache nje ya lango la Mtibwa Sugar

KADI Dk 73, Ndemla analambwa kadi ya njano kwa kumwangusha Barnabas
Dk 71, Kichuya anajaribu kumtoka Tshabalala, anautoa na kuwa kona
SUB Dk 70 Daniel Lyanga anaingia kuchukua nafasi ya Ajib
Dk 65 hadi 70, zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja na hakuna shambulizi hata moja langoni
SUB Dk 64, Mtibwa wanamumtoa Mohammed Ibrahim na nafasi yake inachukuliwa na Vicent Barnabas

Dk 62, Henry Joseph anaruka kama Bruce Lee na kumkanyaga mgongoni Ajib, bahati yake mwamuzi hakuona au amejikausha. Ajib anatolewa nje huku akilia, daktari wa Simba anajaribu kumbembeleza

Dk 59, Simba wanafanya shambulizi kubwa, krosi mbili za Tshabalala na Nimubona unamfikia Ajib, anajitwisha, lakini unatoka sentimeta chache katika lango la Mtibwa Sugar
Dk 58, Said Mohammed anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira safi ambao kama angeuwahi Ajib, ingekuwa hadithi nyingine
SUB Dk 56 Jaffar Kibaya anaingia kuchukua nafasi ya Hussein Javu kwa upande wa Mtibwa Sugar

Dk 52, Baba Ubaya anapiga shuti kali kabisa, linagonga mwamba na kuokolewa
Dk 50, Jeba anaingia eneo la hatari lakini anajiangusha mwamuzi anasema holaaa

Dk 47, Mtibwa Sugar wanaonekana kuanza kwa kasi zaidi na kuwapa Simba wakati mgumu

MAPUMZIKO
+3
Dk 45, Kichuya anajaribu kumtoka Juuko, anamgonga na mkono na mpira unakuwa kona
Dk 45, krosi safi ya Ally Shomari inazua kizazaa kikubwa kwenye lango la Simba, lakini kipa Agbani anafanya kazi ya ziada na kuweka mambo safi

Dk 44, Said Mohammed tena, anafanya kazi ya ziada, anaruka na kuokoa krosi safi ya Ajib
Dk 41, Ibrahim Rajab anapiga shuti kali lakini linambabatiza Mkude na kuokolewa. Mkude analala chini, anatibiwa
Dk 38 krosi safi ya Nimubona, lakini Mtibwa Sugar wanafanya kazi ya ziada na kuokoa. Inakuwa kona lakini isiyo na mafanikio

Dk 37, Said Mohammed, anatoka langoni na kulazimika kuokoa nje
Dk 34, wanarudi kucheza zaidi katikati, mpira unaonekana kupooza sana
Dk 33, Kiiza anapokea pasi safi ya Kazimoto, anaachia mkwaju mkali lakini unatoka sentimeta chache nje ya lango la Mtibwa

SUB Dk 30, Simba inamtoa Mwalyanzi na kumuingiza Said Hamisi Ndemla
Dk 29, Juuko anafanya kazi ya ziada kuokoa krosi ya Kichuya, inakuwa kona ya kwanza kwa Mtibwa na inachongwa na Kichuya lakini haina matunda
Dk 22 hadi 26, zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja, lakini Simba wamefanikiwa kushambulia mara mbili, Mtibwa hawajafanya shambulizi hata moja


KADI Dk 21, Henry Joseph analambwa kadi ya njano kwa kumpiga ngwara Mwalanzi
Dk 19, Said Mohammed anafanya kazi ya ziada kutoka kwa kasi na kuuwahi mpira ambao angechelewa ungesababisha hatari langoni mwake
Dk 17, Jeba anawapangua mabeki wa Simba, lakini Juuko anatokea na kumwangusha, Mtibwa wanapiga faulo lakini haina faida

Dk 16, Mwalyanzi anaingiza krosi safi kabisa baada ya kugongeana na Tshabalala lakini Kiiza anashindwa kuitumia nafasi hiyo vizuri
KADI Dk 12, Justice Majabvi analambwa kadi ya njano kwa kumfanyia madhambi Sheza Kichuya

Dk 9, Ally Shomari anaingia vizuri kabisa katika eneo la hatari lakini anashindwa kupiga krosi nzuri
Dk 7 Nimubona anaingia vizuri lakini anapiga krosi kuubwaaa ambayo haina madhara katika lango la Mtibwa Sugar

GOOOOOO Dk 5 Kiiza anaruka juu na kufunga bao safi kabisa kwa kichwa akiunganisha krosi Tshabalala kutoka kushoto.
Dk 3, kona safi ya Ajib, Said Mohammed anaokoa vizuri kabisa na kuwa kona nyingine, inachongwa na Tshabalala lakini inaokolewa

Dk 2, Tshabalala anaingia na kupiga krosi safi sana, lakini inaokolewa na kuwa kona

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic