January 29, 2016


IDRISSA

Baada ya taarifa za Klabu za Yanga na Simba kulalamika kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya Azam FC kuruhusiwa kushiriki michuano ya nje ya nchi huku Ligi Kuu Bara ikiendelea, Azam imekuja juu na kusema kuwa klabu hizo kongwe zinajiona ni sawa na Miungu watu katika soka la Tanzania.

Azam ipo nchini Zambia ambapo ilipewa ruhusa na TFF ikishiriki mashindano maalumu baada ya kualikwa, ambapo watakaa kwa siku tano kisha kurejea nchini kufuatia ruhusa kutoka TFF.

Katibu Mkuu wa Azam FC, Idrissa Nassor, amesema anashangaa Simba na Yanga kutatizika juu ya safari yao hiyo na kudai wakifanya wao ni sahihi ila siyo wengine.

“Kuna klabu 16 Tanzania lakini hakuna zilizolalamika zaidi ya Simba na Yanga kwa kuwa zenyewe ndizo zinajiona Miungu watu, jambo hili lingekuwa limefanywa na klabu hizi mbili hakuna timu ambayo ingelalamika.

“Azam tumekwenda huko kwa ruhusa maalumu kwa lengo la kuinoa timu yetu ili iweze kuwa katika kiwango kizuri kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ili kupata uzoefu kwani asilimia kubwa ya timu ambazo tunakutana nazo huko ndizo nyingi zinashiriki michuano hii.

AZAM FC WAKISHANGILIA...

“Simba na Yanga zipo kwa muda mrefu katika soka letu na zimeshashiriki mara nyingi katika michuano ya Caf, lakini hakuna chochote walichokifanya kwa maendeleo ya soka letu zaidi ya kuishia katika hatua za awali tu kila mara.


“Hivyo tunahitaji kubadili taswira ya soka letu kwa kuhakikisha tunatengeneza mazingira yatakayotusaidia kufanya vema na kufika mbali ili kuongeza idadi ya timu zitakazoshiriki mashindano haya mwakani,” alisema Idrissa.

3 COMMENTS:

  1. Huyu nae ni walewale,kubadili mfumo kwa kuhonga marefa na TFF,uchafu!

    ReplyDelete
  2. Wamezoea kupanga matokeo nakumbuka mwaka jana alicheza kama leo na mtibwa siku mbili baadae anacheza nae tena moro. Akanunua mechi ya yanga ili sima asishiriki michuano ya kimataifa. Bange mbaya unaweza jukurupuka lisilosahihi ukaliona sahihi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic