January 29, 2016


Amissi Tambwe raia wa Burundi ndiye kinara wa ufungaji mabao katika Ligi Kuu Bara.

Tambwe anayekipiga kwenye kikosi cha Yanga, anaongoza kwa ufungaji akiwa na mabao 13, akifuatiwa na Mganda, Hamis Kiiza wa Simba, mwenye mabao 10, huku Donald Ngoma (Yanga) na Elias Maguri kutoka Stand, wote wakiwa na mabao tisa wakishika nafasi ya tatu na nne.

Tambwe ambaye amefunga hat-trick mbili msimu huu, amesema ataendelea kufunga kila anapopata nafasi ya kufanya hivyo, kwani nia yake ni kuisaidia Yanga na kuchukua tuzo ya ufungaji bora.

“Kila nitakapopata nafasi ya kufunga nitafunga, kwa nini nisifunge wakati ndiyo kazi yangu nikiwa kama straika? Katika mabao yangu, nataka kuisaidia Yanga pamoja na kujiwekea nafasi nzuri ya kutwaa tuzo ya ufungaji bora.

“Nimejipanga kupambana na kila hali ili nitimize lengo langu nililojiwekea msimu huu,” alisema Tambwe, mchezaji wa zamani wa Simba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic