January 25, 2016


Habari njema kwa mashabiki wa Simba, ni kurejea dimbani kwa straika tegemeo, Ibrahim Ajib na winga wa kushoto, Bryan Majwega ambao wamekuwa nje kwa nyakati tofauti, lakini upande wa pili habari mbaya ni Mkenya Paul Kiongera kupata jeraha la msuli.

Ajib amekuwa nje wiki moja tangu aumie kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa wiki mbili zilizopita huku Majwega akiwa hajaonekana tangu aumie kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, lakini wote wanatarajia kuanza mazoezi leo.

Kurejea kwao ni shangwe kwa Wanasimba kwani wanakuja kuboresha safu ya mbele kusaidiana na Amisi Kiiza na Danny Lyanga ambao ndiyo wanaiongoza Simba kipindi hiki.

Taarifa hizo zimethibitishwa na mratibu wa kikosi hicho, Abbas Ally ‘Gazza’, ambaye amesema Kiongera aliumia kwenye mchezo dhidi ya JKT Ruvu, ingawa siyo jeraha kubwa.


“Ajib na Majwega kesho (leo) wanaanza mazoezi ya jumla, Kiongera aliumia msuli katika mchezo uliopita lakini siyo jeraha kubwa la kumuweka nje muda mrefu, huenda naye akaanza muwa wowote,” alisema Gazza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic