Kipa mkongwe wa TP Mazembe, Muteba Kidiaba amesema alitamani kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika anayecheza Afrika hizo kwa kuwa anaendea ukingoni kisoka.
Lakini akakubali kuwa, Samatta alikuwa na nguvu sana na ilikuwa si lahisi kushindwa kutokana na alichokifanya mwaka 2015.
“Ningeshinda ingekuwa jambo jema kwangu, ningefurahi sana. Lakini Samatta alikuwa na nafasi kubwa na ilikuwa ni lazima ashinde, nampongeza kwa kuwa ni mwenzetu na mpiganaji wetu pia ambaye tumepambana pamoja,” alisema Kidiaba akizungumza na waandishi wa habari wa DR Congo mara baada ya kurejea akitokea nchini Nigeria ambako zilifanyika hafla ya tuzo hizo.
0 COMMENTS:
Post a Comment