January 5, 2016


Mshambuliaji Paul Kiongera wa Simba amesema atakaa sawa na kuwa katika kiwango kizuri baada ya kurejea Simba.

"Mpira una mazingira tofauti, kila ninapocheza ninajifunza jambo. Najua baada ya siku chache nitakuwa vizuri," alisema.

Kiongera amesema anahitaji muda kidogo ili kuzoea tena mazingira ya soka nchini ili arudi katika kiwango chake na kucheza vizuri.

Nyota huyo raia wa Kenya, ameshindwa kuonyesha cheche zake katika mechi za kwanza za Ligi Kuu Bara akiwa na Simba. Lakini pia hakung'ara katika mechi ya kwanza ya Mapinduzi Simba ikiivaa Jamhuri na kutoka sare ya mabao 2-2.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic