January 26, 2016


Mshambuliaji Mkenya wa Simba, Paul Kiongera, amepania kutengeneza upya kiwango chake.

Awali alisema amepoteza hali ya kujiamini, lakini baadaye anaamini anahitaji kuongeza stamina na kasi.

“Najitahidi kurejea kwenye kiwango ninachotaka. Kweli tokea nimerudi Simba mambo hayajakaa vizuri, lakini sijakata tamaa,” alisema.

Kiongera ambaye ana sifa ya kuwa msumbufu na mfungaji mzuri, ameonekana kushindwa kucheza katika kiwango bora tokea alipojiunga na Simba kwa mara ya pili akitokea KCB ya Kenya.

KCB ilimuuza Simba, mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya Coastal Union akaumia baada ya kugongana na kipa Shabani Kado. Akapelekwa India kutibiwa na baada ya hapo Simba ikamtoa KCB kwa mkopo ili arejeshe kiwango.


Simba iliamua kumrejesha baada ya Kiongera kuanza kufanya vema akiwa na KCB katika Ligi Kuu ya Kenya. Lakini tokea amerejea nchini na kujiunga na Simba, ameshindwa kuonyesha cheche.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic