January 26, 2016

TWITE (KUSHOTO) NA JUMA ABDUL
Angalau kuna faraja kidogo upande wa Yanga baada ya kiungo mwingine, Mbuyu Twite kufanya mazoezi mepesi leo.

Pamoja na Twite, beki wa kulia, Juma Abdul naye aliungana naye kufanya mazoezi mepesi.

Twite ambaye ni majeruhi, aliungana na wachezaji wengine wa Yanga katika Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo hakufanya mazoezi makali zaidi ya kukimbia taratibu akisindikizwa na Juma Abdul ambaye pia ni majeruhi. Yalipoanza mazoezi makali, akapumzika.


Hivi karibuni, Yanga walipata faraja baada ya kurejea kwa kiungo Haruna Niyonzima aliyekuwa amesimamishwa kwa utovu wa nidhamu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic