January 27, 2016

AGBANI

Siku chache baada ya kuanza kibarua cha kukinoa kikosi hicho, Kocha Mkuu wa Simba Mganda, Jackson Myanja, amemtangaza Muivory Coast, Vicent Angban kuwa kipa namba moja kwenye kikosi chake.

Kocha huyo aliitoa kauli hiyo, hivi karibuni kabla ya mechi ya Kombe la FA dhidi ya Burkina Faso iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri Morogoro, mchezo uliomalizika kwa Simba kushinda mabao 3-0 yakifungwa na Hamis Kiiza (mawili) na Said Ndemla.

MAYANJA
Kocha huyo, tangu ameanza kibarua hicho amekuwa akimtumia Angban katika kikosi cha kwanza katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar waliyoshinda bao 1-0 na JKT Ruvu ambayo waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.


 Mayanja anaona ni sahihi kumtangaza Angban kuwa kipa namba moja kutokana na kutoruhusu nyavu zake kutikiswa kwenye michezo mitatu.
Mayanja alisema, kipa huyo amemshawishi kwa kiwango kikubwa katika mechi hizo mbili za ligi kuu na ile ya FA.

 “Siku zote kipa mzuri na bora ni yule anayejitahidi kuokoa hatari golini kwake kama ilivyokuwa kwa Angban, katika mechi alizocheza amefanya vizuri kwa kudaka na kuokoa hatari nyingi.

“Hivyo basi sioni sababu ya kutoendelea kumtumia Angban katika mechi zijazo za ligi kuu na Kombe la FA kutokana na uwezo wake mkubwa ambao ameendelea kuuonyesha uwanjani,” alisema Mayanja

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic