January 27, 2016

TAMBWE

Mshambuliaji nyota wa Yanga na kinara wa mabao Ligi Kuu Bara, Amissi Tambwe, amesema bado ana safari ndefu kuhakikisha anafanikiwa kutwaa kiatu cha dhahabu mwishoni mwa msimu kutokana na ushindani mkubwa uliopo.

Tambwe amefanikiwa kufunga mabao 13 hadi sasa na kuwa kinara wa mabao huku akimwacha mbali Hamisi Kiiza wa Simba mwenye mabao kumi, Donald Ngoma wa Yanga na Elias Maguri wa Stand United wote wakiwa na mabao tisa kila mmoja.

 Tambwe raia wa Burundi amesema kuwa, anafurahi kuona anaongoza katika ufungaji lakini bado ana kibarua kikubwa mbele kutokana na ushindani uliopo, hivyo anahitaji kujituma zaidi ili kufikia malengo.

“Siku zote napenda kuwa juu ya wengine kuona ninafanikiwa, nimefurahi kuona nina mabao 13 lakini bado nina changamoto kubwa ya kuweza kujituma ili kufanikiwa kukitwaa kiatu hicho.


“Ushindani bado upo mkubwa sana kutokana na kila mchezaji kuhitaji kufanikiwa kuibuka mshindi hivyo kama sitajituma naweza kushindwa kutimiza malengo yangu, mabao niliyonayo siyo mengi sana natakiwa kufunga zaidi,” alisema Tambwe ambaye alikuwa mfungaji bora msimu uliopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic