January 27, 2016


Kiungo Mzimbabwe wa Yanga, Thabani Kamusoko ameweka rekodi ya kuwazidi viungo wengine wa Ligi Kuu Bara katika ufungaji mabao.
Mzimbabwe huyo, hivi sasa anafukuzana kwa mabao na mshambuliaji tegemeo wa Azam FC, John Bocco, mwenye mabao sita baada ya kufunga mabao matano.

Wakati Kamusoko akifunga mabao hayo, kiungo wa Simba Mzimbabwe mwenzake, Justuce Majabvi mwenyewe amefunga mabao mawili huku viungo wengine nyota, Jonas Mkude, Said Ndemla (Simba), Salum Abubakary ‘Sure Boy’ , Himid Mao na Kipre Balou (Azam FC), wakiwa hawana mabao.

Kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao ya faulo, alitua kuichezea Yanga msimu huu wa ligi kuu akitokea FC Platinum ya nchini kwao na kusaini mkataba wa miaka miwili.

Akizungumzia mabao hayo aliyofunga, Kamusoko alisema kuwa: “Nimekuwa nikifunga mabao kutokana na umakini nilionao ndani na nje ya eneo la hatari.
“Jukumu la kufunga mabao siyo la washambuliaji pekee ni letu wote, hivyo kufunga kwangu mabao kuna punguza presha ya washambuliaji,” alisema Kamusoko.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic